Empolyment opportunityJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/E/34 17 Februari, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1).Pamoja na kazi zingine chombo hiki
kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa
Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 517 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama ifuatavyo:
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Katibu Tawala Mkoa Arusha, Katibu
tawala Mkoa Pwani, Katibu tawala Mkoa Simiyu, Katibu tawala Mkoa Katavi, Katibu
tawala Mkoa Iringa, Katibu tawala Mkoa Tabora, Katibu tawala Mkoa Kilimanjaro, Katibu
tawala Mkoa Kagera, Katibu tawala Mkoa Rukwa na Katibu tawala Mkoa Njombe.
Waajiri wengine ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Arumeru, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kiteto, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karatu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Kisarawe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Rufiji, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mafia, Mkurugenzi Halmashauri
ya wilaya ya Mkuranga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Mkurugenzi
Halmashauri ya wilaya ya Kondoa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chamwino,
Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Chemba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya
Mufindi, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Njombe, Mkurugenzi Halmashauri ya
wilaya ya Makambako, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kilosa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Magu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kahama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Maswa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Nafasi hizi pia ni kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ushetu, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Busega, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mkalama, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Igunga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sikonge, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Handeni, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Karagwe, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kyerwa, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Mlele, Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Arusha, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Musoma, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Morogoro na Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Tabora.
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa kwa sharti hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji wanatakiwa kuambatisha maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 03 Machi, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
xvi. Pamoja na waombaji kuainisha waajiri, Sekretarieti ya Ajira baada ya usaili itawapangia waombaji waliofaulu, kwa mwajiri yoyote bila kujali chaguo la mwombaji.Hii ni kutokana na baadhi ya waombaji kupendelea kufanya kazi kwenye baadhi ya maeneo tu.
Katibu, AU Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma, Secretariat,
SLP.63100, P.O.Box 63100
Dar es Salaam. Dar es Salaam.
1.0 AFISA LISHE II (NUTRITION OFFICER II) – NAFASI 21
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali na kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya.
Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine yenye lishe duni.
Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wilaya.
Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya.
Kusimamia kazi za lishe katika wilaya
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajriwa wenye Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi na Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and Nutrition, Food Science and Technology and Food Science) au Stashahada ya juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
2.0 MSAIDIZI LISHE (NUTRITION ASSISTANT) – NAFASI 16
2.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kutambua na kuorodhesha na kuweka kumbukumbu za watoto chini ya miaka mitano na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni ngazi ya kijiji na kata.
Kufuatilia na kutoa ushauri wa lishe kwa kaya zenye watoto wenye lishe duni.
Kuelekeza watoto na makundi mengine yanayoathiriwa na lishe duni wapelekwe kwenye kituo cha afya Kwa huduma zaidi.
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za lishe zinazotolewa kwa makundi mbalimbali kwenye kata/kijiji.
Kukusanya taarifa na takwimu za lishe katika sehemu yake ya kazi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye cheti cha miaka miwili cha mafunzo ya lishe kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali.
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS A kwa mwezi
3.0 MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT)– NAFASI 12
3.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kulea watoto katika vituo vya malezi ya awali ya watoto wadogo mchana.
Kutoa mafunzo kwa akina mama juu ya malezi bora ya awali ya watoto wadogo wenye umri wa miaka 0-8.
Kusaidia shughuli za kinga za magonjwa ya watoto vijijini/sehemu au eneo la vituo.
Kuwa kiongozi wa kituo cha malezi ya awali ya watoto wadogo.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu mafunzo ya mwaka mmoja ya malezi ya awali ya watoto wadogo wenye umri kati ya miaka 0-8 kutoka katika Chuo kinachotambulika na serikali au wenye cheti cha mwaka mmoja cha mafunzo ya ustawi wa jamii.
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS B Kwa mwezi
4.0 AFISA USTAWI WA JAMII II (SOCIAL WELFARE OFFICER II)– NAFASI 184
4.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kuendesha usaili kwa wahudumiwa (watu wenye ulemavu, wazee, familia zenye matatizo, pamoja na watoto na vijana wenye matatizo mbalimbali).
Kufanya ukaguzi wa mazingira wanayoishi wahudumiwa ili kupata taarifa zao kamili.
Kuandaa taarifa za usaili na ukaguzi wa mazingira ya wahudumiwa.
Kupokea na kukusanya taarifa za ustawi wa jamii kutoka kwa wadau na vituo mbalimbali vya ustawi wa jamii.
Kupokea na kukusanya takwimu zinazohusu huduma za watu wenye ulemavu, wazee malezi ya watoto na familia zenye matatizo.
Kupokea kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya uandikishaji wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana, malezi ambao (foster care) na vyuo vya malezi vya watoto wadogo mchana.
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya msaada wa Rais kutoka kwa akina mama waliojifungua watoto watatu au zaidi kwa mara moja.
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi ya watoto yatima au wanaohitaji misaada mbalimbali.
Kupokea, kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
Kuhoji na kuandaa taarifa za washtakiwa.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya B.A (social work or sociology) au stashada ya juu ya Ustawi wa jamii (Advanced Diploma in Sociol work) kutoka chuo cha juu kinachotambuliwa na ustawii wa jamii.
4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
5.0 MSAIDIZI USTAWI WA JAMII DARAJA LA II (SOCIAL WELFARE ASSISTANT II) – NAFASI 24
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutambua na kuhudumia watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
Kukusanya takwimu zinazohusu watu walio katika makundi maalum na mazingira hatarishi.
Kuchambua na kuandaa orodha ya maombi mbalimbali kutoka kwenye familia na watu wenye dhiki.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya mwaka mmoja ya Ustawi wa Jamii kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi.
6.0 MHUDUMU WA JIKONI/MESS DARAJA LA II (KITCHEN/MESS ATTENDANT) – NAFASI 4
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusafisha Vyombo vya kupikia.
Kusafisha Vyombo vya kulia chakula.
Kusafisha Meza itumiwayo kwa kulia chakula.
Kuwatayarishia Wapishi/Waandazi vifaa vya Mpishi na Mezani.
Kusafisha maeneo ya kulia chakula na kupikia.
Kuwasaidia Waandazi na Wapishi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne.
6.3 MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
7.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FORESTRY OFFICER GRADE II) – NAFASI 6
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
Kufanya utafiti wa misitu.
Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
Kukusanya takwimu za misitu.
Kufanya ukaguzi wa misitu.
Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti kwa wananchi.
Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
8.0 MSAIDIZI MISITU DARAJA LA II (FORESTRY ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 75
8.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya mbegu
Kuhudumia na kutunza bustani za miti.
Kutunza na kuhudumia miti na misitu.
Kufanya doria.
Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
Kukusanya takwimu za misitu.
Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.
Kukusanya maduhuli.
Kupima mazao ya misitu.
Kufanya doria.
8.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au Stashahada (Diploma) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
8.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C kwa mwezi.
9.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRICULTURE GENERAL) – NAFASI 10
9.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
9.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agriculture General) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
10.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (AGRONOMY) – NAFASI 4
10.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
10.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Science Agronomy) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
11.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HORTICULTURE) – NAFASI 1
11.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
11.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Horticulture) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
12.0 MKUFUNZI KILIMO DARAJA LA II (HUMAN NUTRITION) – NAFASI 1
12.1 KAZI NA MAJUKUMU
Kusoma na kuelewa vema mihutasari ya mafunzo na kuitafsiri kwenye masomo.
Kuandaa mtiririko na mpangilio wa masomo (lesson sequences and plans) kwa upande wa nadharia na vitendo.
Kufundisha kozi za Stashahada na Astashahada nadharia na vitendo.
Kuandaana kufundisha kozi za Wakulima.
Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao.
Kupima maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo wa Wilaya/Viwandani wakati wa mafunzo kwa vitendo (Field Practical).
Kutekeleza shughuli nyingine za kikazi kadri atakavyopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
12.2 SIFA ZA KUINGILIA MOJA KWA MOJA
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Kilimo (Bachelor of Human Nutrition) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu kozi ya mbinu bora za kufundishia (Teaching Methodology)
12.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
13.0 AFISA KILIMO DARAJA LA II (AGRO – OFFICERS) – NAFASI 71 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuthibiti visumbufu vya mazao na mimea,
Kukusanya takwimu za bei za mazao kila wiki na kila mwezi,
Kukusanya takwimu za upatikanaji wa mazao katika masoko kila wiki/kila mwezi,
Kuendesha mafunzo ya wataalam wa kilimo,
Kufanya ukaguzi wa ubora na matumizi ya pembejeo na zana,
Ufuatiliaji wa mwenendo wa soko la mazao ya biashara,
Kuendesha mafunzo juu ya hifadhi bora ya udongo na maji,
Kutoa habari juu ya teknolojia mpya kwa wadau,
Kuandaa/kuandika taarifa za utekelezaji kwa sekta ndogo ya mazao,
Kusimamia/kuendeleza taaluma ya uzalishaji mboga, matunda, maua na mazao mengine,
Kusimamia/kuendeleza uzalishaji wa mbegu bora,
Kuandaa, kutayarisha kufunga na kusambaza mbegu bora,
Kufanya majaribio ya magonjwa kwenye mbegu,
Kufanya ukaguzi wa mbegu mpya kwa kushirikiana na watafiti wa mbegu kabla ya kupitishwa,
Kuendesha mafunzo ya kuzalisha mboga, matunda, maua na viungo,
Kuhamasisha uzalishaji wa mazao ya bustani,
Kufanya utafiti mdogo wa mazao yanayofaa kulimwa katika sehemu ya kilimo cha umwagiliaji,
Kufanya utafiti wa udongo,
Kuhamasisha uanzishaji wa vikundi vya wakulima/wamwagiliaji,
Kuzalisha mbegu za msingi baada ya kuzalishwa na watafiti,
Kuendesha/kusimamaia vishamba vya majaribio vya mbegu na uchunguzi maabara ili kuondoa utata juu ya mbegu.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya kilimo au shahada ya sayansi waliojiimarisha katika mchepuo wa kilimo kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D Kwa mwezi.
14.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 38 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,
Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
15.0 MUUNDA BOTI DARAJA II (BOAT BUILDER II) – NAFASI 2 (LINARUDIWA)
KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusaidia kuunda boti za uvuvi
Kuwashauri wavuvi juu ya utunzaji na matumizi ya boti
Kufanya matengenezo ya boti.
Kusaidia kutafsiri/kusoma michoro ya kiufundi ya boti.
Kuandaa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa boti.
15.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye stashahadaya Uundaji boti kutoka chuo cha Mbegani au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
15.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
16.0 DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II (FERRY / BOAT OPERATOR) – NAFASI 1 (LINARUDIWA) KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
MAJUKUMU YA KAZI
Kufunga na kufungua kamba za kivuko.
Kuchunga usalama wa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.
Kupanga abiria au magari kwenye kivuko.
Kuendesha na kuongoza kivuko.
Kutunza daftari za safari ya kivuko.
Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
16.1 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye mashua/vivuko.
16.2 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
17.0 AFISA MIFUGO DARAJA LA II (LIVE STOCK OFFICER II) – NAFASI 8
(LINARUDIWA). KWA WALE WOTE WALIOOMBA TANGAZO LA TAREHE 27 NOVEMBA 2013 WASIRUDIE KUOMBA KWA KUWA MAOMBI YAO BADO YANACHAMBULIWA.
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
Atabuni mipango ya uzalishaji mifugo wilayani.
Ataratibu uzalishaji wa mifugo katika mashamba makubwa ya mifugo.
Atasaidia kuratibu mipango ya ugani kuhusiana na uzalishaji wa mifugo wilayani.
Ataratibu na kuendesha mafunzo ya ufugaji bora, usindikaji wa mazao ya mifugo kwa wataam wa mifugo na wafugaji.
Atafanya mapitio na marekebisho ya miundo ya masoko ya mifugo wilayani kwake na mkoani.
Atabuni, kuanzisha na kutekeleza miradi ya maendeleo ya mifugo wilayani.
Atafanya soroveya ya rasilimali (resource survey) kama vile mifugo, vyakula vya mifugo, malisho n.k. katika eneo lake la kazi.
Ataendesha mafunzo kwa Mawakala, wauzaji na wataalam juu ya njia salama katika kuweka na kusambaza pembejeo za mifugo.
Atatafiti maeneo mapya yanayofaa kwa ufugaji wa mifugo mbalimbali
Atafanya utafiti juu ya uharibifu wa mazingira katika wilaya.
Atashiriki katika shughuli za kudhibiti milipuko ya wanyama/viumbe waharibifu wa malisho.
Ataandaa taarifa ya jumla juu ya maendeleo ya mifugo.
Atafuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uzalishaji wa mifugo.
Atafanya kazi nyingine zinazohusiana na fani yake kama atakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
17.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (bachelor degree) ya sayansi ya Mifugo(Animal Science) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali au sifa inayolingana nayo.
17.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi
18.0 MHASIBU MSAIDIZI (ASSISTANT ACCOUNTANT) - NAFASI 3
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kupokea na kulipa fedha.
Kutunza daftari ya fedha.
Kufanya usuluhisho wa hesabu za benki
Kukagua hati za malipo.
Kupitisha malipo kulingana na kanuni za fedha.
Kusimamia kazi za wasaidizi wa hesabu.
18.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha kufaulu mtihani mgumu wa Uhasibu Serikalini (Higher Standard Government Accountancy Examination) unaotolewa na Tume ya Utumishi wa Umma. Au
Kuajiriwa wenye Stashahada ya kawaida ya uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyyote inayotambuliwa na serikali.
18.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi
19.0 AFISA USHIRIKA DARAJA LA II (COOPERATIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukagua vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyoendesha miradi ya pamoja ( Jointy Venture )
Kuhamasisha uanzishaji wa vyama vya Ushirika vya Msingi.
Kukusanya na kuchambua takwimu zinazohusu Masoko katika Mkoa.
Kutoa ushauri juu ya uendeshaji wa Vyama vya Ushirika vya Msingi
Kuratibu/kushiriki katika Elimu ya Ushirika Shirikishi katika vyama vya ushirika vya Msingi.
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza au Stashahada ya Juu (Advanced Diploma) katika fani ya Ushirika (Cooperative management and accounting) kutoka vyuo vinavyotambulika na Serikali.
19.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
20.0 AFISA UGAVI DARAJA LA II (SUPPLIES OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kukusanya takwimu za kusaidia kutayarishwa makisio ya vifaa vinavyohitajika (Material Requirement Budget) na Mpango wa Ununuzi (Procurement Plan).
Kukusanya na kutunza takwimu za utendaji za Wazabuni mbalimbali.
Kukusanya na kutunza takwimu za upokeaji, utunzaji, na usambazaji wa vifaa.
Kusimamia utunzaji wa maghala na hati/kumbukumbu ya vifaa vilivyomo ghalani.
Kusimamia upokeaji, utunzaji na usambazaji wa vifaa (Physical Distribution).
Mfumo wa uwekaji na utunzaji wa vifaa ghalani (Location Index Design).
Kusimamia ukaguzi wa kuhesabu vifaa mara kwa mara (Perpetual Stock Checking) ghalani.
Kutayarisha Taarifa za kazi katika vipindi maalumu.
Kuhesabu na kutoa taarifa ya thamani ya vifaa vilivyomo ghalani kila mwisho wa mwaka (Annual Stock Taking).
Kufanya kazi zingine ambazo atapangiwa.
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Biashara (B.Comm) yenye mchepuo wa ugavi au Stashahada ya Juu ya Ugavi (Advanced Diploma in Materials Management) inayotolewa na Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya usimamizi wa Vifaa.
20.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D mwezi.
21.0 AFISA UGAVI MSAIDIZI II (ASSISTANT SUPPLIES OFFICER) – NAFASI 1
21.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutunza ghala la vifaa lenye thamani ndogo.
Kupokea vifaa vipya vitakavyoletwa na wazabuni mbalimbli na kupokea vifaa ambavyo vimetumika lakini vinahitaji kutunzwa kabla ya kufutwa.
Kufungua na kutunza “Bin Card” kwa kila kifaa kilichopo ghalani.
Kufungua “Ledger” ambayo itatunza kumbukumbu ya vifaa vinavyoingia, kutunzwa na kutoka kwa nyaraka mbalimbali.
Kutoa vifaa kwa wateja na watumiaji wengine.
Kuhakikisha kwamba ghala na vifaa vilivyomo vinatunzwa katika hali ya usafi na kwa usalama.
Kuandaa hati za kupokelea vifaa.
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa.
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye cheti cha “National Store-Keeping Certificate au “Foundation Certificate” kitolewacho na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa au wenye Cheti kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
AU
Kuajiriwa wenye Diploma ya Kawaida “Ordinary Diploma in Materials Management” kutoka Chuo kinachotambuliwa na Bodi ya Taifa ya Usimamizi wa Vifaa.
21.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.A na B kwa mwezi.
22.0 AFISA UTAMADUNI II (CULTURAL OFFICER GRRADE II) – NAFASI 1
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutafiti masuala ya Lugha, Sanaa, Mila na Desturi katika ngazi ya Wilaya.
Kufundisha fani mbalimbali za utamaduni katika Vyuo na Vituo vya Elimu na mafunzo ya utamaduni.
Kazi nyingine atakazopangiwa na Mkuu wa kituo.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada au stashahada ya juu katika Sanaa, Lugha au Sayansi ya Jamii na uzoefu wa kazi usiopungua miaka mitatu.
22.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
23.0 AFISA MAENDELEO YA VIJANA DARAJA LA II (YOUTH DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuratibu na kisimamia utekelezaji wa Sera ya Vijana
Kuratibu shughuli za mikopo/mifuko ya Vijana
Kuhamasisha vijana ili kufufua moyo wa kujitolea nchini
Kupanga na kuendesha mafunzo yanayohusu stadi za maisha, stadi za kazi na Afya ya Vijana
Kuanzisha vituo vya ushauri nasaha, Ajira kwa Vijana na Elimu ya Familia kwa kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali (NGO)
Kukusanya takwimu mbalimbali zinazohusu Vijana
Kuratibu shughuli mbalimbali za NGO zinazoshughulikia masuala ya Vijana
Kuandaa mipango ya kuboresha malezi ya Vijana
Kuwahamasisha Waajiri na Wafadhili mbalimbali wachangie mfuko wa mikopo nafuu kwa Vijana katika maeneo mbalimbali
Kukuza na kuendeleza vipaji mbalimbali walivyonavyo Vijana ili kuwawezesha kujiajiri
Kuandaa mipango ya kuwahamasisha Vijana ili kuanzisha miradi midogomidogo ya kujiajiri.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza (BA. in Sociology or Social Sciences) au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii au Ustawi wa Jamii au Maendeleo ya Vijana (Advanced Diploma in Social Works or Community Development or Youth Development) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serkali.
23.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
24.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
24.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
24.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
25.0 AFISA ARDHI DARAJA LA II (LAND OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
25.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kusimamia uingizaji wa kumbukumbu katika kompyuta.
Kushughulikia utayarishaji wa nyaraka za kisheria.
Kufanya ukaguzi wa viwanja.
Kutoa notisi na kupendekeza ubatilishaji wa miliki kwa visivyoendelezwa kwa mujibu wa sheria.
Kuwasiliana na wateja kuhusu Hati zilizotayarishwa na kuwakabidhi.
25.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Usimamizi ardhi na Uthamini au Shahada ya Sheria kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitano.
25.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
26.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - KOMPYUTA (COMPUTER TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 1
26.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
26.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Waliohitimu kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani yenye muelekeo wa kompyuta
Waliohitimu kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya kompyuta
Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani yenye muelekeo wa kompyuta katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
26.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
27.0 AFISA BIASHARA DARAJA LA II (TRADE OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
27.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuwasiliana na Wizara nyingine ambazo zinafanya biashara, kupata takwimu ambazo zitatumika katika kutathimini mwenendo wa biashara na masuala mengine ya kibiashara.
Kusambaza taarifa za kibiashara kwa wafanyabiashara.
Kutathmini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko katika nchi mbalimbali ambazo bidhaa zetu zinauzwa.
Kuandaa grafu na “chart” ambazo zinaonyesha, mwenendo wa bidhaa zinazoingizwa nchini na zile ziendazo nje kwa kila nchi ambazo hufanya biashara na Tanzania.
27.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Biashara waliojiimarisha katika fani ya Uchumi, Masoko, Uendeshaji Biashara au inayolingana nayo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salam au chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali.
27.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
28.0 MSAIDIZI WA HESABU (ACCOUNTS ASSISTANT) - NAFASI 1
28.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandika na kutunza “register” zinazohusu shughuli za uhasibu.
Kuandika hati za malipo na hati za mapokezi ya fedha.
Kutunza majalada yenye kumbukumbu za hesabu
Kupeleka barua/nyaraka za uhasibu Benki.
Kufanya usuluhisho wa masurufu, karadha, Hesabu za Benki na Amana.
28.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Cheti cha ATEC level II au “Foundation Level” kinachotolewa na NBAA
28.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
29.0 AFISA USIMAMIZI WA FEDHA DARAJA LA II (FINANCE MANAGEMENT OFFICER II) - NAFASI 1
29.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandikisha na kudhibiti Amana (Securities) za Serikali.
Kufuatilia hati za hisa.
Kuwasiliana na watoaji mikopo/misaada kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa miradi.
Kuweka kumbukumbu za madeni ya nje.
Kuweka kumbukumbu za mikopo ya ndani.
Kufuatilia na kusimamia matayarisho ya makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali.
Kufuatilia utayarishaji na uchambuzi wa “Flash Reports” za kila mwezi.
29.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Uchumi na Mipango (Major in Economics) au Biashara au Sheria (LL.B) au Stashahada ya Juu ya Uhasibu au Uchumi & Mipango au Biashara au Stashahada ya juu ya Usimamizi wa kodi kutoka Chuo/Taasisi inayotambuliwa na Serikali.
Waombaji wenye Cheti cha Taaluma ya Uhasibu CPA (T) au sifa nyingine inayolingana na hiyo inayotambuliwa na NBAA watafikiriwa kwanza.
29.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
30.0 AFISA TARAFA – NAFASI 6
30.1 MAJUKUMU YA KAZI
(i) Kwenye Mamlaka ya Serikali Kuu.
Kumwakilisha na kumsaidia Mkuu wa Wilaya katika utekelezaji wa shughuli za Serikali Kuu katika Tarafa.
Kuandaa na kuratibu taarifa na ripoti zinazohusu masuala ya ulinzi na usalama ya kata kwenye tarafa yake na kuiwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kuhamasisha na kuhimiza wananchi iliwashiriki kwenye shughuli za maendeleo kwenye Tarafa.
Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Wananchi Katika Tarafa.
Kuwa mlinzi wa amani katika eneo lake.
Kufuatilia na kuhimiza utekelezaji wa sera za Serikali katika eneo lake na kuhakikisha kuwa zinatekelezwa ipasavyo.
Kuratibu shughuli zote za maafa na dharura mbalimbali katika eneo lake
Kuandaa taarifa zote zinazohusu masuala ya Serikali Kuu kuhusu utendaji wa kazi za maafisa Watendaji wa kata wa eneo lake na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya.
Kuwa kiungo kati ya Serikali kuu na Serikali za Mitaa. katika eneo lake.
Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Katibu Tawala wa Wilaya.
(ii) Kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kuwasaidia Wakurugenzi wa Serikali za Mitaa katika shughuli za Maendeleo katika eneo lake
Kusimamia utendaji wa shughuli za Maafisa Watendaji wa Vijiji, Kata na Mitaa.
Kushiriki na kutoa ushauri katika upangaji wa mipango ya Maendeleo katika eneo lake
Kuhudhuria vikao vya kamati za Halmashauri na Baraza la madiwani na kutoa ushauri.
Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake kama zitakavyopokelewa kutoka kwa Watendaji wa Kata.
Kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa au Jiji.
30.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Sheria,Menejimenti,Utawala,Sayansi ya Jamii, Kilimo, Mifugo,Ushirika, Mazingira, au Maji kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
30.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS D kwa mwezi.
31.0 AFISA MICHEZO DARAJA LA II (GAMES AND SPORTS OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
31.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufundisha fani mbalimbali kwa Waalimu wa vyuo, shule, na vituo vya Elimu na Mafunzo
Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa waalimu, Makocha, viongozi wa vyama na vilabu vya michezo
Kufundisha fani mbalimbali za michezo kwa Timu za Michezo mbalimbali.
31.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada au Stashahada ya Juu ya Elimu ya Michezo (Physical Education) kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali.
31.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
32.0 FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI (TECHNICIAN GRADE II - (MAPPING) – NAFASI 1
32.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushughulikia madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza kumbukumbu zake
Kutunza kumbukumbu za “cadastrals surveys” na mahesabu yake
Kuandaa nakala za “cadastral site plans”
Kutunza miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
32.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani (Mapping)
32.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
33.0 FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) – NAFASI 1
33.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya maandalizi ya Uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika
Kutunza kumbukumbu za ramani na plan
Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji
Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji
33.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya ufundi ya miaka miwili au Stashahada katika fani ya Urasimu Ramani (Cartography) kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
33.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
34.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - MAJI - (TECHNICIAN GRADE II - WATER) – NAFASI 1
34.1 MAJUKUMU YA KAZI
Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
Kutunza takwimu za maji
Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro
Kuchora hydrograph za maji
Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k.
Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
Kuingiza takwimu kwenye kompyuta
Kufundisha wasoma vipimo
34.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
34.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
35.0 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 1
35.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kutekeleza Kazi za Ushirikishaji Wadau Katika Uhifadhi.
Kudhibiti Utoaji wa Leseni za Biashara Za Nyara na Vibari vya Kukamata Wanyama Hai.
Kushiriki Katika Kusuluhisha Migogoro ya Matumizi ya Wanyamapori
Kudhibiti Matumizi Haramu ya Leseni za Uwindaji na Kuhahakikisha Kufuatwa Kwa Maadili Katika Kutumia Wanyamapori.
Kuthibiti Matumizi Haramu ya Wanyamapori.
Kufuatilia Utekelezaji wa Miongozo Mbalimbali ya Uhifadhi Wanyamapori.
Kuhakiki Viwango vya Kukamata Wanyama Hai Kwa Ajili ya Biashara na Ufugaji.
Kufanya Kazi za Kuzuia Ujangili.
Kukusanya Taarifa, na Takwimu za Uhifadhi.
Kutekeleza Kazi za Uhifadhi Katika Mapori ya Akiba.
35.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa Wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori Kutoka Chuo Kikuu Kinachotambuliwa na Serikali.
35.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi
36.0 AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 2
36.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja hili watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria Waandamizi ikiwa ni pamoja na:
Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.
36.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
36.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi
X. M. Daudi
Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
It is the blog that triggers you to arouse entrepreneurship spirit. It aims at strenghthening the people through psychological treatment by inspiring the readers to plan for their better destiny. Generally it is the site Dedicated to provide psychological and entrepreneurship consultancy. CONTACTS: P.O.BOX 355 HANDENI, TANZANIA +255712135799 gkanjara@gmail.com
CONSTITUTIONA WRITING
-
Empolyment opportunity JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA Kumb. Na EA.7/96/01/E...
-
Constitution for small entrepreneurship groups it is the set of rules and agreement that facilitate and guides the operation...
-
Knowing your strength it is one of the step for moving into the road of success. Your strength it specifically focus on under...
Tuesday, February 18, 2014
Sunday, January 19, 2014
ELIMU NA HATIMA YA TANZANIA
Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo mfumo wa elimu umeshindwa kuleta mabadiliko ya kweli ya kujenga taifa linalojitegemea. Tusipokuwa makini itakuwa vigumu kujenga taifa la watu wanaojitambua na hatimaye kuendelea kuwa na kizazi cha watumwa wa ukoloni mambo leo. Sishangai kwa hatua ya serikali kuruhusu walioshindwa kufikisha viwango vya ufaulu mtihani wa kidato cha pili 2013, kuruhusiwa kuendelea na masomo ya kidato cha nne. Haya yote yanatokea kutokana na kutokuwa na falsafa madhubuti inayoongoza wizara ya elimu kama itikadi ya nchi. Mara nyingi mtizamo wa maendeleo ya elimu hapa nchini kwetu imekuwa ni kuongeza uandikishaji wa wanafunzi wanaohudhuria kuanzia shule ya msingi hadi vyuo vikuu huku kipimo cha elimu kikiwa ni ufaulu wa vyeti.
Miongozo mbalimbali ikiwemo MKUKUTA sura ya tatu inazungumzia maisha bora na ustawi wa jamii lengo namba tatu linaelezwa kuwa ni upatikanaji wa elimu bora ya msingi na sekondari kwa wasichana na wavulana, elimu ya watu wazima kwa wote miongoni mwa wanawake na wanaume na upanuzi wa elimu ya juu na elimu ya ufundi. Dhana hii imejengwa katika kuongeza idadi na suala la ubora na wanafunzi wa sampuli gani halijapewa kipaumbele. Kwa mfano taarifa ya utekelezaji wa MKUKUTA 2009/2010 iliyotolewa na wizara ya fedha na uchumi inasema kuwa kumekuwepo ongezeko kuhusu maendeleo ya elimu kwa kutaja takwimu ambazo kimsingi ni vigumu kupima ubora wake na mchango wa maendeleo ya ongezeko hilo kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Taarifa hii na nyingine nyingi zitolewazo kwa kufata mwongozo wa MKUKUTA kwa mtizamo wangu naona siyo sahii kupima ubora wa maendeleo ya elimu Tanzania bali mchango wa wanafunzi wanaohitimu uwe ndio kipimo cha maendeleo hapa nchini. Kipimo cha ubora kiende sambamba na jinsi ongezeko la wahitimu na kupungua kwa matatizo mbalimbali ya kijamii. Fikra ile ile ya kuangalia takwimu imejipenyeza hata kwenye Mpango wa matokeo makubwa sasa (Big Results Now) ambao kwa upande wa elimu, Halmashauri zimepewa jukumu la kutumia rasilimali chache walionazo kuhakikisha ufaulu unaongezeka. Wakati haya yakiendelea wanazuoni mbalimbali wamekuwa wakihoji kuhusu mitaala inayofundishwa Tanzania kuwa inawajenga wanafunzi kukariri na sikuwa wadadisi na wagunduzi wa mambo mbalimbali yenye kuleta tija kwa taifa letu.
Tanzania imeruhusu watu wanaopewa nguvu ya kuongoza wizara kila mtu kuja na mpango wake ambao unakuwa na maneno tofauti lakini ukichambua kwa kina mfiumo inayoweza kuleta fikra mpya kwa wanafunzi haibadiliki. Kibaya zaidi ni enzi za Mheshimiwa Joseph Mungai aliyefuta masomo ya kilimo kwa shule za sekondari na wakati inajulikana kabisa asilimia 80 ya watanzania wanaishi vijijini na uchumi wao mkubwa unaotegemewa ni kilimo. Tangu mvurugano huu kujitokeza nchi imekuwa ikirudi nyuma kila kukicha. Si sera wala viongozi wapya wanaopewa dhamana wanabadili kitu isipokuwa kufanya marekebisho yakushusha viwango vya ufaulu ilimradi wanafunzi wengi waendelee na ngazi za juu zaidi huku wakiwa hawakidhi vigezo.
Elimu imefwanywa bidhaa kama unavyoweza kununua sokoni huku ikijenga makundi miongoni mwa watanzania. Wale wenye kuaminika kuwa na ukwasi mwingi wao wanajitenga na watoto wa masikini kwa kusoma shule maalum zinazolipiwa ghrama kubwa. Watoto wa maskini wameundiwa shule maalum za kata ambazo nimara chache kukuta watoto wa viongozi wakubwa kama mawaziri , viongozi na matajiri. Pamoja na mgawanyiko huo hamanishi kwamba wanaokwenda shule za binafsi wanapata elimu bora kwani wanajengwa katika mazingira yakuweza kufaului kupata vyeti vizuri vya kuwawezesha kuingia soko la utumwa wa karne ya 21 ambayo ni kuajiriwa. Mwalimu Nyerere kwenye miaka ya 1964 alianzisha falsafa ya elimu ambayo ililenga taifa linalojitegemea kwa kusisitiza elimu ya kujitegemea. Kuwajengea uwezo wa Tanzania kuweza kuvuna rasilimali zao wenyewe kuliko ilivyo sasa Tanzania haina wataalamu wakuvuna rasilimali zetu kama gesi, madini na nyingine zinazoendelea kugunduliwa katika maeneo mbalimbali ya nchi. Tumeshindwa kuwajenga Watanzania kuwa na uwezo wa technolojia ambayo imepelekea rasilimali muhimu kukabidhiwa kwa makampuni mengi ya kigeni ambayo yanachukua faida kubwa itokanayo na rasilimali zetu kuliko kama tungetumia wataalamu wetu -waiosomeshwa kwa kodi zetu. Hata tunaowaita wataalam wamekuwa watumwa wa utaalam wao.
Tumekimbizana na utandawazi wa kuruhusu wawekezaji wa nje kwa misingi kwamba dunia imekuwa kijiji kimoja. Lakini kwa kufanya hivyo tumeshindwa kuwa na majibu kuwa ni Watanzania wangapi wanauwezo wa kuwekeza katika mataifa makubwa , wanawekeza katika nini na taifa linanufaikaje.Kwa kufanya hivyo soko tumeliacha lijiendeshe bila kuangalia nafasi yetui katika utandawazi. Mwaka 1998 wakati Mwalimu Nyerere anatunukiwa shahada ya heshima kutoka chuo kikuu huria cha Tanzania alisema "....... as we prepare ourselves for a competitive life in the Global village, we must not forget that our corner stone is going to be in rural Tanzania or the informal sector of urban Tanzania.
Watunga sera tulionao wamekuwa watu wakukopi na kupesti pamoja kupokea mshinikizo ya wafadhili kutoka nchi za magharibi bila kuangalia uwezekano wa kutekeleza mifumo ya kimagharibi katika jamii ya Kitanzania. Watu wanafikiri kama vile vijiji vya Tanzania hawavijui. Lakini kwa hili si shangai linatokana na watu kupewa vitengo ambavyo hawana weledi navyo. Hauwezi ukawa na mchumi peke yake au mtu aliyebobea kwenye mitaala ya elimu bila kumhusisha msosholojia ambaye amebobea katika uchambuzi wa sera za kijamii na mchango unaotolewa na sera husika katika kuboresha maisha ya watu. Kwa uchambuzi wa kisosholojia unaenda mbali zaidi kutathmini utofauti wa aliye hitimu la saba na yule ambaye hajafika kabisa, tofauti kati ya kidato cha nne na darasa la saba na aliyehitimu chuo kikuu na aliyehitimu stashahada. Tusipoweza kung'amua ubora na michango ya watu hawa hata kama udahili utaongezeka mara mia huku hauendani na majibu ya changamoto zinazoikumba jamii ni viogumu kusema kuwa elimu imeboreshwa Tanzania.
Mao Tse Tung katika kitabu chake 1966 (selected speeches ) anatufundisha umuhimu wakujifunza kutokana na makosa. Hivyo kukosea kwa binadamu kupo tukubali tuna paala tulikosea ndio maana tumeendelea kuwa na utegemezi wa teknolojia katika uvunaji rasilimali zetu na kuendelea kuzalisha wasomi ambao ni watumwa wa kuajiriwa na kushadadia wazungu.
TUFANYE NINI?
Kutokana na ukweli kwamba elimu hii imekuwa ikipigiwa kelele marakwa mara bila majibu na kwa kuwa watu wengi wamesoma lakini bado wameendelea kuwa watumwa wa elimu zao sambamba na nchi kuendelea kutegemea wataalam na makampuni ya nje nashauri mambo yafuatayo kufanyika ili kuleta mabadiliko ya kweli na kujega taifa imara linalojitosheleza kifkra na kiteknolojia mambo yafuatayo yafanyike.
Kuwepo na mtizamo na falsafa mpya yakuongoza wizara ya elimu kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu. Tunahitaji falsafa ambayo itapandikiza chachu ya wasomi kujitegemea na kuja na mabo mapya. Kwamfano kama sasa mtu anasoma ili kuajiriwe kwenye taasisi kubwa basi mwanafunzi aanze kusoma akiwa na fikra ya kutengeneza fursa yakuajiri na kulipa mishaara mikubwa. Pia mwanafunzi ajengwe kutodharau kazi na kutoingiliwa na wanasiasa katika harakati za kujitafutia maisha ilimradi havunji sheria.
Pili kama taifa tuwe na vibaumbele katika elimu inayotolewa huku misingi mikuu ikiwa ni kuwa na wataalamu wa uzalishaji katika kilimo waliojiari wenyewe na serikali itoe fursa na maeneo maalumu kwa vijana watakaohitimu wakataka kujikita katika kilimo. Kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa na kinaweza kuajiri watu wengi. Hivyo katika mabadiliko ya falsafa na dhana ya elimu, somo la kilimo liwe la lazima kuanzia darasa la awali huku likihuisha na mazingira yetu. Wataalam wa saikolojia wanasema mwanafunzi ukimfundisha katika mambo yanayoendana na mazingira pamoja na vitendo anaelewa haraka na kuthamini ujuzi anao pewa. Kwa hili kuna baadhi ya shule nimejifunza kwa mfano shule ya Sekondari Weruweru katika maadhimisho ya miaka 50, wameonyesha kitu cha utofauti wanafunzi wana muda wa kwenda shamba na shamba kweli ukiliona linaonyesha lipo kwenye taasisi ya elimu kutokana na ubora wake. Siyo hilo tu bali ata utashi kwa wanafunzi ni mkubwa kujisomea na kufanya kazi. Kama taarifa zilizokuwa zinarushwa na kituo cha chaneli ten ni za kweli basi kama wizara ina haja yakushirikisha uzoefu wa shule hii katika kuimarisha sera na miongozo ya elimu Tanzania.
Tukiachana na kilimo pia tunahaja yakufanya tathmini ni wapi tunapwaya kiteknolojia ili tuweze kuwaandaa vijana wa Kitanzania kusoma fani ambazo zina umuhimu katika kuvuna rasilimali za nchi yetu. Tuitafute teknolojia popote pale duniani hasa katika mambo ya gesi, mafuta, madini na teknolojia ya umwagiliaji ili tusiwe wasindiokizaji katika utandawazi. Kama viongozi wanaweza kusafiri nje kwa safari zisizo na tija iweje ishindikane kila mwaka kupeleka vijana wakitanzania zaidi ya 50 kila mwaka kuisaka teknolojia. Ili kuhakikisha tunaondokana na kukimbiwa na wataalam tuliowasomesha (brain drain), tuwasainishe mikataba ambayo itawafanya kurudi nyumbani baada ya masomo. Sambamba na hilo tuwe na makampuni ya serikali yaliyojikita kwa kila sekta kama gesi, mafuta nk. ili ikitokea nchi anawahitaji wataalam wetu serikali iwe inalipya kwa kuwatumia wataalam watakaosomeshwa na kodi za Watanzania (consultancy services).
Tukisha kuwa na hawa wataalamu tuwape kinga wasiingiliwe na wanasiasa maana ndio chanzo cha kushusha morali na uzalendo kwa wataalam. Hata asiyekuwa na ABC kwenye kitu fulani anajifanya kuwa anajua kila kitu na kuzalilisha taaluma za watu wengine. Tukiwawezesha vijana kusoma fani ambazo zina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa nchi ni sehemu moja wapo ya kutoa hamasa kwa vijana wengi wa Kitanzania kupenda masomo ya sayansi. Ili kufanikisha hili, kwa kuanza serikali inatatakiwa kuwa na na shule maalum kuanzia msingi zitakazojengwa katika itikadi na mchepuo wa ujuzi fulani ili hatimaye wakiendelea na masomo ya juu zaidi wawe na msingi imara na isiwe kusubiri mtu amalize kidato cha sita alafu aende kwenye fani fulani. Nimetumia neno serikali makusudi tusiiachie sekta binafsi maana sekta binafsi inalenga kwenye faida na inaweza kutoa mwanya kwa wenye pesa pekee kuwa ndio wanufaika wakuu wa programu hii. Kwangu mimi sioni kama haiwekani kama tukiwa na utashi wa kisiasa, uzalendo na utaifa badala yakujikita katika vyama vya siasa vinavyopambana kutawala dola na si taifa linalojitegemea.
Tatu kufanya mabadiliko katika upatikanaji wa wataalam wa sera na utafiti kuhusu mambo ya elimu. Lazima kuwepo na wasosholojia na wataalam wengine hasa walijikita katika mambo ya elimu. Tukiwa na watunga sera kutoka fani moja ya elimu au wachumi bila wasosholojia bado kupata falsafa na dhana ya elimu tuitakayo itakuwa ndoto.
Nne mfumo wa ufundishaji uwe wa vitendo zaidi kuliko nadhalia ili wanafunzi kujengewa uwezo wa kuweza kutumia uzoefu kubuni vitu vipya na vyenye tija kwenye jamii kuliko ilivyosasa ambapo mwanafunzi anakesha akisoma ilikufikisha viwango vya ufaulu vilivyowekwa huku akiwa na fikra mgando katika kung'amua mambo. Msomi cheti kwa sasa hana nafasi kwa kipindi ilikuwa enzi hizo.Tubadilike ilikuendana na kasi ya utandawazi na kujinasua na ukoloni mambo leo ambao tusipokuwa makini utaimaliza Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Tano tuache tabia za kubebana kukabidhi majukumu makubwa kwa watu amabo hawana maono wala utashi-watu ambao wanalewa madaraka . Kuna watu wanapopewa vitengo anajiona kana kwamba yeye ni Tanzania one katika hiyo fani kumbe wengine ni kwasababu tu yakuwa karibu na watawala na kama kumngekuwepo na uwanja wa wazi kushindania nafasi hiyoasingeweza kutamba. Kupewa na fasi bado unafursa kutumia mawazo ya wanaofikria zaidi yako kufanya mabadiliko. Wengine, wakishapata, hudharau waliochini yao suala ambalo siyo sahii. Elimu siyo mchezo wa timu moja bali nishirikishi-tunahitaji kuchanganya mawazo, kupingana kwa hoja na hatimaye kujenga muafaka na hatimaye kuwa na mtizamo mmoja kama nchi.
Mwisho nchi ni yetu sote matunda mabaya ya mfumo wa elimu yanamathiri kila mtu hivyo tuungane kuboresha. Lakini katika kuboresha siasa zetu chafu tuweke pembeni tuwe na mwafaka wa nchi na falsafa moja. Hii itatusaidia kuzuia waziri mpya au chama kipya kitakochoingia madarakani kuvuruga elimu yetu na hatimaye kuwa na mfumo bora ambao unazalisha wasomi wenye tija katika taifa.Tangia sasa kubebana iwe mwiko kwa kila mtu. Tukisha kuwa na mmwafaka katika elimu basi naamini ata shule zetu, mfumo wakupata walimu na mazingira yakujisomea yataboreshwa. Lakini tukiendelea elimu kuifanya agenda yakisiasa tunachezea uchumi wa nchi yetu na kuroga maendeleo yetu wenyewe. Maisha tunaishi kwa sasa yaelimu isiyo na tija baada ya miaka kumi iwe ni historia kwani tukifanya haya mabadiliko yatapatikana.
HAYO NI MAWAZO YANGU. NAOMBA KUWASILISHA.NA HAYAWAKILISHI TAASISI AU MWAJIRI WANGU.
Godfrey Vedasto
Mshauri na mchambuzi wa sera za kijamii
07121357/0789915677
Wednesday, January 1, 2014
WATU HATARI
Kuna watu wa ajabu wenye mambo ya kushangaza katika dunia hii. Kutokana na imani yangu Mungu tunaye mmoja na ndiye anayestaili kuabudiwa. Lakini wanadamu baadhi wamejifanya kuwa miungu watu kutokana na sababu kubwa mbili. Sababu ya kwanza msingi wake unatokana na kuwa na mamlaka juu ya watu wengine. Mamlaka yamewanya baadhi ya watu wawadharau wengine hadi kuwadhalilisha utu wao. Sababu ya pili ni kuwa na umiliki wa mali (rasilimali pesa). Kuna baadhi ya watu wanataka kuabudiwa na kujiona kwamba kila wanachosema ni sahihi kuliko wengine. Sababu nyingine ambayo kwa sasa haina nguvu sana ni elimu. Kwamaana unaweza ukawa na elimu lakini kama hauna mamlaka ya kiutawala au pesa au kuwa karibu na watawala unaweza usiwe na nguvu katika dunia ya sasa. Lakini pamoja na hayo kuna watu wanotumia mwanya wa ujinga wa watu kuwatawa kifikra hali ambayo utengeneza umungu MTU.
Hali hii yakutaka kuabudiwa imekuwa ndiyo chanzo cha migogoro mbalimbali inayoendelea hapa duniani. Ukichambua kwa kina utaona hawa watu wanaojiona bora zaidi ya wengine ni wale ambao hofu ya Mungu haipo ndani ya mioyo yao. Makundi haya yamwshika hatamu si kwenye siasa bali hata kwenye majumba ya ibada kama makanisa na misikiti. Ndiyo wanaopewa kipaumbele kwa mambo mengi.
Pia watu wanojiona bora zaidi ya wenzao huwa na sifa ya ubinafssi. Ukimkuta ofisini mali ya umma anaitumia kama vile ni mali yake. Mtu wa sampuli hii ni mwepesi kuchukua hatua kali kwa waliochini yake pindi wanapokosea huku akisahau maovu ambayo anayafanya yeye mwenyewe. Akiachishwa cheo huwa siyo wepesi wakuonyesha ushirikiano bali huwa na majungu na ni hatari kwani wanaweza kufanya mbinu zozote zile mbaya amabzo zinaweza kumhatarisha mtu mwingine aliyepewa hiyo nafasi.
Mara nyingi hawa watu wakujikweza na kupenda kuabudiwa, huwa ni wanafiki ikiwa na maana kwamba hupenda kuonekana wasafi mbele za watu kwa gharama zozote iwe kwa kutumia cheo au pesa ili mradi jamii iwaone wanafaa. Watu hawa, vigumu kuleta mabadiliko kani wao wenyewe hawajabadilika (not transformed therefore it is difficult to transform others).
Kutokana na tabia za watu hawa husababisha migogoro kujitokeza kati yao na jamii. Kwa mfano mwenye mamlaka akiwadharau waliochini yake hawatamheshimu na matokeo yake kama ni wafanya kazi utafuta sababu na mbinu za kumwonyesha kwamba hawamkubali. Kwa kufanya hivyo migogoro upamba moto.
Kwa mwenye pesa utaka kumiliki kila nyenzo muhimu katika maisha ikiwa ni pamoja kupanga bei sokoni na kudhulumu rasilimali za wanyonge. Na wanyonge wakijitambua wakaona wanafanyiwa ndivyo sivyo upambana kwa migomo na maandamano kwa maana sheria mara nyingi huwa upande wa mwenye pesa na hata akiwa na kosa mamlaka zinazohusika umwajibisha kifallme suala amabalo huchochea migogoro kwa wananchi.
Ukikosa hofu ya Mungu kama binadamu inapelekea mtu kutokuwa na hekima na busara matokeo yake ni kutoa maamuzi kwa misingi yakutaka kujiona bora zaidi na kudharau wengine kwa misingi ya fedha, elimu na nafasi/ mamlaka aliyonayo mtu. Pia hali hii huchochea kutotendeka kwa haki na ibinadamu hatimaye migogoro. Wanadamu wamekengeuka mpaka kufikia hatua ya kuwajeruhi watu wengine kimwili na kiroho ambao harakati zao zinapingaukiukwaji wa haki za binadamu na unyonyaji.
Hali hii yakutaka kuabudiwa imekuwa ndiyo chanzo cha migogoro mbalimbali inayoendelea hapa duniani. Ukichambua kwa kina utaona hawa watu wanaojiona bora zaidi ya wengine ni wale ambao hofu ya Mungu haipo ndani ya mioyo yao. Makundi haya yamwshika hatamu si kwenye siasa bali hata kwenye majumba ya ibada kama makanisa na misikiti. Ndiyo wanaopewa kipaumbele kwa mambo mengi.
Pia watu wanojiona bora zaidi ya wenzao huwa na sifa ya ubinafssi. Ukimkuta ofisini mali ya umma anaitumia kama vile ni mali yake. Mtu wa sampuli hii ni mwepesi kuchukua hatua kali kwa waliochini yake pindi wanapokosea huku akisahau maovu ambayo anayafanya yeye mwenyewe. Akiachishwa cheo huwa siyo wepesi wakuonyesha ushirikiano bali huwa na majungu na ni hatari kwani wanaweza kufanya mbinu zozote zile mbaya amabzo zinaweza kumhatarisha mtu mwingine aliyepewa hiyo nafasi.
Mara nyingi hawa watu wakujikweza na kupenda kuabudiwa, huwa ni wanafiki ikiwa na maana kwamba hupenda kuonekana wasafi mbele za watu kwa gharama zozote iwe kwa kutumia cheo au pesa ili mradi jamii iwaone wanafaa. Watu hawa, vigumu kuleta mabadiliko kani wao wenyewe hawajabadilika (not transformed therefore it is difficult to transform others).
Kutokana na tabia za watu hawa husababisha migogoro kujitokeza kati yao na jamii. Kwa mfano mwenye mamlaka akiwadharau waliochini yake hawatamheshimu na matokeo yake kama ni wafanya kazi utafuta sababu na mbinu za kumwonyesha kwamba hawamkubali. Kwa kufanya hivyo migogoro upamba moto.
Kwa mwenye pesa utaka kumiliki kila nyenzo muhimu katika maisha ikiwa ni pamoja kupanga bei sokoni na kudhulumu rasilimali za wanyonge. Na wanyonge wakijitambua wakaona wanafanyiwa ndivyo sivyo upambana kwa migomo na maandamano kwa maana sheria mara nyingi huwa upande wa mwenye pesa na hata akiwa na kosa mamlaka zinazohusika umwajibisha kifallme suala amabalo huchochea migogoro kwa wananchi.
Ukikosa hofu ya Mungu kama binadamu inapelekea mtu kutokuwa na hekima na busara matokeo yake ni kutoa maamuzi kwa misingi yakutaka kujiona bora zaidi na kudharau wengine kwa misingi ya fedha, elimu na nafasi/ mamlaka aliyonayo mtu. Pia hali hii huchochea kutotendeka kwa haki na ibinadamu hatimaye migogoro. Wanadamu wamekengeuka mpaka kufikia hatua ya kuwajeruhi watu wengine kimwili na kiroho ambao harakati zao zinapingaukiukwaji wa haki za binadamu na unyonyaji.
Monday, November 18, 2013
SEXUAL HARRASMENT FOR WOMEN IN PUBLIC OFFICE -TANZANIA
Sexual harassment in different public offices has been a great challenge facing women especially the first appointment one .Various studies that are done concentrates on women who are in rural areas and those employed in public offices are not considered. According to my experience and information from different women blaming heads of department for their behavior of harassing them sexually I were to take initiative to interview women who have experienced such harassment and positions of men who are commonly known for that injustice behavior.
Prepared by G.Vedasto
Social welfare consultant
gkanjara@gmail.com
0789915677
The methods I used to get information from different respondents were to interview women from two departments such as health and community Development. The reason for using these departments is due to the fact that those two are the leading to have employed more women in comparison with other departments. I took 6 women from Community Development and 6 women from Health department in one of the district in Tanga regeion. Then the information I got used to be terms of reference from other two district in different region.
The findings in this research were firstly attributed on the group that is highly affected between the new women employee and the old one. The second point of observation was the positions of men in public offices who have more preference in harassing women. The third one was the pressure that makes women to accept harassment and their silence of not reporting anywhere once they are sexually harassed.
For the group which is highly affected the new employee women were found to be the victim of sexual harassment when compared with the old one at a certain working place. The reason is that because of being tranger, perpetrators of women rights sticks on new comers and every perpetrator struggles to be the first in having sex with new employees. After comparative analysis with other districts in Tanzania this was found to be the same in many areas particularly where heads of departments are men. Bad enough after having gone with a women perpetrator are proud themselves as they think it is prestige to have sex with new employee.
The position for the perpetrators of w omen's rights most of them are heads of departments and units who are supervisors of new employees and the one responsible for placing them into working stations.According to women interviewed the findings shows that every one said were approached by average of five heads of departments. This situation is terrible and endangering the health of women especially new entrants in public offices in different districts in Tanzania. Human resources officers are found to be the leading in practicing such unbelievable acts when comparing with other heads of departments. Despite the legislation of special act to monitor the behavior of public servants which make illegal the use of position for sexual gain.
The expression from women interviewed said that at the time of their reporting time different heads of departments called them through their phone and directed them to specific guest house promising to pay for them all costs because new employee in most cases are the strangers in areas where are placed at the first time. Others called upon new entrants in employment to accept them sexually so that their allowance could be paid fast so as to rescue them from living in hard condition. According to guidelines of employment in Tanzania depending on your salary level , a person is to be paid seven days allowances which in some areas are intentionally paid late or not paid totally. This makes the environment for some heads of departments and units to influence women to be sexually harassed.
According to evidence from respondents interviewed most of women said that despite of those illegal acts done to them they keep silence because first they expect to be placed in good working station especially town areas. The nature of geography in rural areas it is to terrible-not attractive for new entrants of employment due to the fact that most of them where brought up in rural areas and experiencing hardship of important services. Therefore they keep silence in spite of being sexually harassed so as to enjoy innovative and digitalized services that are predominant in town areas.
Also others said that keep silence because it is difficult to report they bosses as there is no clear confidentiality mechanism that can protect them.Once bosses are aware of some one being reported for sexual harassment may recommend poorly in their files that can affect status for promotion. For others to make cheap themselves in the eyes of the boss they think of having much privilage in the offices which many have proved being betrayed by their boss when are not fulfilled. Most of bosses after enjoying sexuall rewards they change their minds-no long needs to continue with relationship.
Those facts above were found to have occurred in many local government offices in Tanzania. I tried to conduct comparative analysis with my friends especially women who have newly employed in public service in Tanzania. Although this study was conducted in public sector it does not mean that women in private sector are safe. Women are exposed in different harassment from interview and appointment for the job. I call upon women activist to have increased and re innovating intervention approaches that can integrate safety of all women wherever they are.'My friend sexual harassment for us (women) is very high. You can not believe these heads of departments who are highly respected they have behavior that devalue their position and makes us (women) not respect them. There men who are very common in harassing every new employee (woman)' These are words from one of respondents during the interview.
Prepared by G.Vedasto
Social welfare consultant
gkanjara@gmail.com
0789915677
Thursday, October 24, 2013
PSYCHOLOGICAL SUPPORT TO MVC
The picture shows children enjoying the celebration of Afrcan Child Day that captured much attention to children as they played drama and brought opportunity to meet with children from different areas.
Monday, September 30, 2013
WAZEE WETU TUWAENZI
Ndugu wapendwa katika Bwana , tarehe 1/10/2013 ni maadhimisho ya siku wazee. Kwa hapa nchini kwetu yanafanyikia Korogwe mkoani Tanga. Katika madhimisho hayo wazee kutoka mikoa mbalimbali wataungana kusherehekea siku hii ya muhimu sana. Natoa wito kwa Watanzania kuwaunga mkono kwa kufanya mambo yenye utofauti ambayo kwayo upendo unaweza kujidhihirisha. Wazee hawa ni tunu na wana mengi ambayo sisi kama vijana tunajifunza kwao. Wazee hawa wana mchango mkubwa katika kutujenga kifikra na kimawazo kwani kuishi kwao kwingi wameona mengi na wanayo mengi tunayojifunza kutokana na uzoefu wao.
Nashauri mambo yafuatayo katika kuwakumbuka wazee ili waweze kuona utofauti na siku zote
Kwanza tujitolee kuwasaidia wazee ambao hawana msaada kabisa walau kuwafanyia shughuli yoyote kwa mfano kuwafulia nguo, kuwachotea maji au chochote kile ambacho unaona unaweza kukifanya.
Pili, tuwapigie simu kwa wale ambao wako mbali . Hali hii itawafanya wafurahi na kuona kuwa jamii/ndugu wanawasamini. Pia katika maongezi yetu iwe kwa njia ya simu au uso kwa uso yaambatane na utani waweze kuburudika na kupunguza msongo wa mawazo. Katika jamii zetu kuna baadhi ya wazee wanaokosa watu wa kuwatania hivyo wanajisikia vibaya kama wametengwa na jamii.
Tatu tuwaombee ili Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa nguvu za kimwili na kiroho. Tunajua wazee wetu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali hivyo tukiwa karibu nao kwa njia ya dua kila mtu kwa imani yake naamini tutaweza kuimarisha mioyo yao na hatimaye kuendelea kuwa na afya njema huku wajukuu na vitukuu wakiendelea kunufaika kutokana na busara na baraka za wazee wetu.
Nne, kwa watunga sera na vyombo mbalimbali vya maamuzi sasa vione haja yakutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha ustawi ulio bora kwa wazee. Wazee wasitajwe kwa misingi ya kujizolea umaharufu kisiasa bali tunapowataja kweli iwepo ndani ya mioyo yetu hata matendo yadhirishe tunayyatamka. Imezoeleka wakati wa chaguzi watu ndo huwaona wazee wa maana wakishapata ndo basi tena. Kama tunawapangia bajeti tuhakikishe fedha za miradi ya wazee zinakuja kwa wakati.
Tano, kama jamii ipangwe mikakati mahususi ya kuwasaidia wazee wasio na uwezo kupitia serikali zetu za vijiji au mitaa. Tusiwaache wenyewe maana kila mtu anaelekea uzeeni. Kwa kadili watoto watakavyoona wazee wanavyotunzwa na jamii tutakuwa tumetengeneza mnyororo wa uhakika wa hifadhi ya jamii kwa wazee. Kuanzia ngazi ya familia isiwe huyu ni babu mdogo au bibi mdogo wote hawa ni ndugu zetu baraka zao nikubwa katika mafaniko yetu. Inashangaza kuona watu wako mijini wanakula starehe huku babu, bibi , shangazi, mjomba hata wazazi wao wanateseka vijijini. Kunauwezekano ugumu wa maisha na kutofanikiwa ni laana inayotokana na kutowajali wazee.
Mwisho nina imani tukiyazingatoia haya tutaweza kuwa na jamii inayowathaminini wazee. Lakini la muhimu zaidi tukiawajali wazee tunaweza kuongeza miaka ya kuishi kwani mtu akifika uzeeni hatakuwa na msongo wa mawazo, hatajisikia mpweke bali atakuwa na nguvu na utulivu wa akili hivyo kumpunguzia magonjwa kama ya moyo ambayo yanaweza kusababishwa na kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kinga ya kijamii endelevu na yenye uhakika kwao.
Imeandaliwa na:
Afisa Ustawi wa Jamii na mshauri wa kisaikolojia
HANDENI-TANGA
E-mail :gkanjara@gmail.com
0712135799
Nashauri mambo yafuatayo katika kuwakumbuka wazee ili waweze kuona utofauti na siku zote
Kwanza tujitolee kuwasaidia wazee ambao hawana msaada kabisa walau kuwafanyia shughuli yoyote kwa mfano kuwafulia nguo, kuwachotea maji au chochote kile ambacho unaona unaweza kukifanya.
Pili, tuwapigie simu kwa wale ambao wako mbali . Hali hii itawafanya wafurahi na kuona kuwa jamii/ndugu wanawasamini. Pia katika maongezi yetu iwe kwa njia ya simu au uso kwa uso yaambatane na utani waweze kuburudika na kupunguza msongo wa mawazo. Katika jamii zetu kuna baadhi ya wazee wanaokosa watu wa kuwatania hivyo wanajisikia vibaya kama wametengwa na jamii.
Tatu tuwaombee ili Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa nguvu za kimwili na kiroho. Tunajua wazee wetu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali hivyo tukiwa karibu nao kwa njia ya dua kila mtu kwa imani yake naamini tutaweza kuimarisha mioyo yao na hatimaye kuendelea kuwa na afya njema huku wajukuu na vitukuu wakiendelea kunufaika kutokana na busara na baraka za wazee wetu.
Nne, kwa watunga sera na vyombo mbalimbali vya maamuzi sasa vione haja yakutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha ustawi ulio bora kwa wazee. Wazee wasitajwe kwa misingi ya kujizolea umaharufu kisiasa bali tunapowataja kweli iwepo ndani ya mioyo yetu hata matendo yadhirishe tunayyatamka. Imezoeleka wakati wa chaguzi watu ndo huwaona wazee wa maana wakishapata ndo basi tena. Kama tunawapangia bajeti tuhakikishe fedha za miradi ya wazee zinakuja kwa wakati.
Tano, kama jamii ipangwe mikakati mahususi ya kuwasaidia wazee wasio na uwezo kupitia serikali zetu za vijiji au mitaa. Tusiwaache wenyewe maana kila mtu anaelekea uzeeni. Kwa kadili watoto watakavyoona wazee wanavyotunzwa na jamii tutakuwa tumetengeneza mnyororo wa uhakika wa hifadhi ya jamii kwa wazee. Kuanzia ngazi ya familia isiwe huyu ni babu mdogo au bibi mdogo wote hawa ni ndugu zetu baraka zao nikubwa katika mafaniko yetu. Inashangaza kuona watu wako mijini wanakula starehe huku babu, bibi , shangazi, mjomba hata wazazi wao wanateseka vijijini. Kunauwezekano ugumu wa maisha na kutofanikiwa ni laana inayotokana na kutowajali wazee.
Mwisho nina imani tukiyazingatoia haya tutaweza kuwa na jamii inayowathaminini wazee. Lakini la muhimu zaidi tukiawajali wazee tunaweza kuongeza miaka ya kuishi kwani mtu akifika uzeeni hatakuwa na msongo wa mawazo, hatajisikia mpweke bali atakuwa na nguvu na utulivu wa akili hivyo kumpunguzia magonjwa kama ya moyo ambayo yanaweza kusababishwa na kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kinga ya kijamii endelevu na yenye uhakika kwao.
Imeandaliwa na:
Afisa Ustawi wa Jamii na mshauri wa kisaikolojia
HANDENI-TANGA
E-mail :gkanjara@gmail.com
0712135799
Sunday, September 29, 2013
TRUE LOVE
Mapenzi ya kweli kwa unayempenda ni nguzo muhimu katika kujenga taifa la watoto wasio wa mitaani. Kama watu mnapendana ni vigumu kuachana. Kikubwa zaidi kama una mpenzi wako jitahidi kuwa muwazi kwake ili ajenge imani na wewe. Jadili pamoja panapotokea jambo la kutatiza. Pia kuwa makini siri au madhaifu ya mpenzi wako usimwambie mtu yeyote maana akifahamu atapoteza imani na wewe. Kuna wengine midomo haina breki hasa vijana wenzagu. Kitendo cha kumwaga siri za ndani unatengeneza mwanya wa wengine kuingilia penzi lenu.
Achana na tamaa, rizika kwa kile unachokipata. Siku hizi watu wanatamaa akiona rafiki yake mpenzi kamnunulia kitu kizuri basi huanza fujo kwa mpenzi wake na kumdharau eti kwa kuwa hajafanyiwa kama rafiki yake- huo ni ulimbukani kwani anyepanga riziki ni Mungu. Kama shida ni gari kaa na mpenzi wako ili mpange mkakati wa kuwawezesha kupata hicho unachokihitaji. Mkipanga pamoja na mkafanikiwa kukipata ukiwa na mwenzi wako faida zake ni nyingin kwanza ni heshima katika jamii, pili mpenzi wako atakuthamini sana na kuona wewe wa maana sana katika maisha.
Acha kuwasifia wapenzi wa watu wengine mbele ya mpenzi wako. halii hii yakusifia wapenzi wa wengine inamfanya mpenzi wako akuone kama bendera fuata upepo hivyo unaweza kumjengea mazingira mpenzi wako asiwe na imani na wewe.
Tumia maneno ya upole pale kuna potokea kukwaruzana na katika kutafuta mwafaka msiwe kama mechi ya kutafuta mshindi bali jishushe tabasamu kidogo, mshike ata shavu mwenzio ili kujengana kiaiokolojia. Kuna wengine mbinu hizi hawazitumii ndio maana wanaweza kununiana hadi mwaka na hatimaye kuachana. Na kama wamezaa pamoja basi watoto huumia kwani hupelekea wakose malezi ya upande mmoja. Kila siku kuwa na hali kama ile ile ya mwanzo wa mahusiano wakati mnatongozana. Nina amini mkifanya hivyo migogoro ya ndoa na kutelekezwa watoto ambako kunapelekea kuongezeka kwa watoto wa mtahani na mmomonyoko wa maadili kutapungua kwa kiwango kikubwa.
Achana na tamaa, rizika kwa kile unachokipata. Siku hizi watu wanatamaa akiona rafiki yake mpenzi kamnunulia kitu kizuri basi huanza fujo kwa mpenzi wake na kumdharau eti kwa kuwa hajafanyiwa kama rafiki yake- huo ni ulimbukani kwani anyepanga riziki ni Mungu. Kama shida ni gari kaa na mpenzi wako ili mpange mkakati wa kuwawezesha kupata hicho unachokihitaji. Mkipanga pamoja na mkafanikiwa kukipata ukiwa na mwenzi wako faida zake ni nyingin kwanza ni heshima katika jamii, pili mpenzi wako atakuthamini sana na kuona wewe wa maana sana katika maisha.
Acha kuwasifia wapenzi wa watu wengine mbele ya mpenzi wako. halii hii yakusifia wapenzi wa wengine inamfanya mpenzi wako akuone kama bendera fuata upepo hivyo unaweza kumjengea mazingira mpenzi wako asiwe na imani na wewe.
Tumia maneno ya upole pale kuna potokea kukwaruzana na katika kutafuta mwafaka msiwe kama mechi ya kutafuta mshindi bali jishushe tabasamu kidogo, mshike ata shavu mwenzio ili kujengana kiaiokolojia. Kuna wengine mbinu hizi hawazitumii ndio maana wanaweza kununiana hadi mwaka na hatimaye kuachana. Na kama wamezaa pamoja basi watoto huumia kwani hupelekea wakose malezi ya upande mmoja. Kila siku kuwa na hali kama ile ile ya mwanzo wa mahusiano wakati mnatongozana. Nina amini mkifanya hivyo migogoro ya ndoa na kutelekezwa watoto ambako kunapelekea kuongezeka kwa watoto wa mtahani na mmomonyoko wa maadili kutapungua kwa kiwango kikubwa.
Wednesday, September 25, 2013
Subscribe to:
Posts
(
Atom
)