CONSTITUTIONA WRITING

Monday, September 30, 2013

WAZEE WETU TUWAENZI

   Ndugu wapendwa katika Bwana  , tarehe 1/10/2013 ni maadhimisho  ya siku wazee. Kwa hapa nchini kwetu yanafanyikia Korogwe mkoani Tanga. Katika madhimisho hayo wazee kutoka mikoa mbalimbali wataungana  kusherehekea siku hii ya muhimu sana. Natoa wito kwa Watanzania kuwaunga mkono kwa kufanya mambo yenye utofauti ambayo kwayo upendo unaweza kujidhihirisha. Wazee hawa ni tunu na wana mengi ambayo sisi kama vijana tunajifunza kwao. Wazee hawa wana mchango mkubwa katika kutujenga kifikra na kimawazo kwani kuishi kwao kwingi wameona mengi na wanayo mengi tunayojifunza kutokana na uzoefu wao.
     Nashauri mambo yafuatayo katika kuwakumbuka wazee ili waweze kuona utofauti na siku zote
Kwanza tujitolee kuwasaidia wazee ambao hawana msaada kabisa walau kuwafanyia shughuli  yoyote kwa mfano kuwafulia nguo, kuwachotea maji au chochote kile ambacho unaona unaweza kukifanya.
    Pili, tuwapigie simu kwa wale ambao wako mbali . Hali hii itawafanya wafurahi na kuona kuwa jamii/ndugu wanawasamini. Pia katika maongezi yetu iwe kwa njia ya simu au uso kwa uso  yaambatane na utani waweze kuburudika na kupunguza msongo wa mawazo. Katika jamii zetu kuna  baadhi ya wazee wanaokosa watu wa kuwatania hivyo wanajisikia vibaya kama wametengwa na jamii.
      Tatu tuwaombee ili Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa nguvu za kimwili na kiroho. Tunajua wazee wetu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali  hivyo tukiwa karibu nao kwa njia ya  dua kila mtu kwa imani yake naamini tutaweza kuimarisha mioyo yao na hatimaye kuendelea kuwa na afya njema huku wajukuu na vitukuu wakiendelea kunufaika kutokana na busara na baraka za wazee wetu.
     Nne, kwa watunga sera  na vyombo mbalimbali vya maamuzi sasa vione haja yakutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha ustawi ulio bora kwa wazee. Wazee wasitajwe kwa misingi ya kujizolea umaharufu kisiasa bali tunapowataja kweli iwepo ndani ya mioyo yetu hata matendo  yadhirishe tunayyatamka. Imezoeleka wakati wa chaguzi watu   ndo huwaona wazee wa maana wakishapata ndo basi tena. Kama tunawapangia bajeti tuhakikishe fedha za miradi ya wazee zinakuja kwa wakati.
       Tano, kama jamii ipangwe mikakati mahususi ya kuwasaidia wazee wasio na uwezo kupitia serikali zetu za vijiji au mitaa. Tusiwaache wenyewe maana kila mtu anaelekea uzeeni. Kwa kadili watoto watakavyoona wazee wanavyotunzwa na jamii tutakuwa tumetengeneza mnyororo wa uhakika wa hifadhi ya jamii kwa wazee. Kuanzia ngazi ya familia isiwe huyu ni babu mdogo au bibi mdogo wote hawa ni ndugu zetu baraka zao nikubwa katika mafaniko yetu. Inashangaza kuona watu wako mijini wanakula starehe huku babu, bibi , shangazi, mjomba hata wazazi wao wanateseka vijijini. Kunauwezekano ugumu wa maisha na kutofanikiwa  ni  laana inayotokana na kutowajali wazee.
       Mwisho nina imani tukiyazingatoia haya tutaweza kuwa na jamii inayowathaminini wazee. Lakini la muhimu zaidi tukiawajali wazee tunaweza kuongeza miaka ya kuishi kwani mtu akifika uzeeni hatakuwa na msongo wa mawazo, hatajisikia mpweke bali atakuwa na nguvu na utulivu wa akili hivyo kumpunguzia magonjwa kama ya moyo ambayo yanaweza kusababishwa na kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kutokuwa na kinga ya kijamii  endelevu na yenye uhakika kwao.

Imeandaliwa na:
Afisa Ustawi wa Jamii na mshauri wa kisaikolojia
HANDENI-TANGA
E-mail :gkanjara@gmail.com
0712135799

Sunday, September 29, 2013

TRUE LOVE

          Mapenzi ya kweli kwa unayempenda ni nguzo muhimu katika kujenga taifa la watoto wasio wa mitaani. Kama watu mnapendana ni vigumu kuachana. Kikubwa zaidi kama una mpenzi wako jitahidi kuwa muwazi kwake ili ajenge imani na wewe. Jadili pamoja panapotokea jambo la kutatiza. Pia kuwa makini siri au madhaifu ya mpenzi wako usimwambie mtu yeyote maana akifahamu atapoteza imani na wewe. Kuna wengine midomo haina breki hasa vijana wenzagu. Kitendo cha kumwaga siri za ndani unatengeneza mwanya wa wengine kuingilia penzi lenu.
         Achana na tamaa, rizika kwa kile unachokipata. Siku hizi watu wanatamaa akiona rafiki yake mpenzi kamnunulia kitu kizuri basi huanza fujo kwa mpenzi wake na kumdharau eti kwa kuwa hajafanyiwa kama rafiki yake- huo ni ulimbukani kwani anyepanga riziki ni Mungu.  Kama  shida ni gari kaa na mpenzi wako ili mpange mkakati wa kuwawezesha kupata hicho unachokihitaji. Mkipanga pamoja na mkafanikiwa kukipata  ukiwa na mwenzi wako faida zake ni nyingin kwanza ni heshima katika jamii, pili mpenzi wako atakuthamini sana na kuona wewe wa maana sana katika maisha.
       Acha kuwasifia wapenzi wa watu wengine mbele ya mpenzi wako. halii hii yakusifia wapenzi wa wengine inamfanya mpenzi wako akuone kama bendera fuata upepo hivyo unaweza kumjengea mazingira mpenzi   wako asiwe na imani na wewe.
      Tumia maneno ya upole pale kuna potokea kukwaruzana na katika kutafuta mwafaka msiwe kama mechi ya kutafuta mshindi bali jishushe tabasamu kidogo, mshike ata shavu mwenzio ili kujengana kiaiokolojia. Kuna wengine mbinu hizi hawazitumii ndio maana wanaweza kununiana hadi mwaka na hatimaye kuachana. Na kama wamezaa pamoja basi watoto huumia kwani hupelekea wakose malezi ya upande mmoja. Kila siku kuwa na hali kama ile ile ya mwanzo wa mahusiano wakati mnatongozana. Nina amini mkifanya hivyo migogoro ya ndoa na kutelekezwa watoto ambako kunapelekea kuongezeka kwa watoto wa mtahani na mmomonyoko wa maadili kutapungua kwa kiwango kikubwa.